Pinned Tweet
Umoja wa Mataifa ni jukwaa pekee linaloleta pamoja mataifa yote, makubwa kwa madogo, kujenga maono ya mustakabali wetu wa pamoja.
Wiki iliyopita, viongozi walihutubia dunia kupitia #UNGA.
Kama anavyosisitiza @antonioguterres: “Umoja wa Mataifa hauna mbadala.”
Kampuni 9 kubwa zaidi za mafuta zilipata faida ya dola bilioni 95 katika miezi 3 pekee.
@antonioguterres anazitaka serikali kutoza kodi faida hizo kubwa za ziada ili kusaidia nchi zilizo hatarini zaidi.
“Wanaochafua mazingira lazima walipe.”
un.org/sg/en/content/sg/stat….
📸 Kumbukumbu ya 2015: Leonardo DiCaprio akiunga mkono #ClimateAction katika mkutano wa tabianchi mjini Paris.
Leo, tunamtakia heri ya siku ya kuzaliwa Balozi huyu wa Amani wa Umoja wa Mataifa. un.org/en/messengers-peace/l…
Ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa #COP31 unatarajiwa kuanza hivi punde, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa @antonioguterres akishiriki.
📺 Fuatilia moja kwa moja: webtv.un.org/en/asset/k1f/k1…
“Juhudi za vijana wa leo za kuleta mabadiliko zinanipa matumaini ya siku zijazo.”
- @antonioguterres, aliyekutana na vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani katika mkutano wa #COP31 kusikiliza hoja na mapendekezo yao kuhusu hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Sudan: Watu milioni 15.4 wanahitaji makazi na vifaa vya msingi, lakini uhaba wa fedha unaruhusu kusaidia mtu 1 tu kati ya 10.
Ufadhili zaidi unahitajika ili Umoja wa Mataifa na washirika wake wawafikie wengi zaidi.
Kupitia @UNHCR
#KeepEyesOnSudan
Sayansi hutusaidia kukabiliana na magonjwa, mabadiliko ya tabianchi na changamoto nyingine.
Katika Siku ya Sayansi Duniani kwa ajili ya Amani na Maendeleo, tunahimiza uwekezaji endelevu katika sayansi kwa mustakabali bora wa wote.
un.org/en/observances/world-…
Joto duniani si takwimu tu. Linaathiri afya, chakula na maisha yetu.
@WMO inaonya kuwa 2026 ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa, huku El Niño ikitarajiwa kuongeza hatari za hali mbaya ya hewa mwaka 2027. wmo.int/news/media-centre/st…
#StateOfClimate
Sayansi inatusaidia kuelewa dunia tunamoishi na kujenga mustakabali bora kwa wote.
Katika Wiki ya Kimataifa ya Sayansi na Amani, tunaangazia umuhimu wa sayansi na teknolojia katika kujenga na kudumisha amani duniani.
Fahamu zaidi: un.org/en/observances/world-…
Mkutano wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa #COP31 unaanza leo Antalya, Uturuki.
Kwa nini ni muhimu kwako?
Chakula, maji, nishati na athari za ukame na mafuriko ni miongoni mwa masuala yanayohusiana na maamuzi ya mkutano huu.
Fahamu zaidi: un.org/en/climatechange/cop3…
🪔 #दीपावली की शुभकामनाएं!
Heri ya Diwali kwa wote wanaosherehekea!
Tunawatakia sikukuu yenye furaha, amani na matumaini. Nuru ya Diwali iangaze mioyo yetu na kuimarisha upendo, mshikamano na umoja miongoni mwetu.
Lugha ya haki za binadamu ni ya ulimwengu mzima.
Haina mipaka.
Haina vizuizi.
Haijalishi unatoka wapi au wewe ni nani, katika kila kona ya dunia, haki hizi ni zako na haziwezi kujadiliwa wala kubadilishwa.
Fahamu kazi ya @UNHumanRights: ohchr.org/en/ohchr_homepage
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yameua watu wasiopungua 30 na kujeruhi takribani 59 huko Abyei, eneo linalogombaniwa na Sudan na Sudan Kusini.
Umoja wa Mataifa unaonya kuhusu vitisho vipya vya usalama na kutoa wito wa uchunguzi huru. news.un.org/en/story/2026/11…
Amani na afya ya sayari yetu vina uhusiano wa karibu.
Katika miaka 60 iliyopita, 40% ya migogoro ya ndani ya nchi imehusishwa na unyonyaji wa maliasili.
Ijumaa ni Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Unyonyaji wa Mazingira Wakati wa Vita na Migogoro ya Silaha.
kupitia @UNEP
#Tanzania: Haki za binadamu zimejadiliwa UN.
Nchi 105 zilitoa maoni katika Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR) ya @UN_HRC, yaliyohitimishwa hivi karibuni.
Ripoti ya mapitio hayo inatarajiwa kupitishwa tarehe 13 Novemba.
Angalia hapa: webtv.un.org/en/asset/k13/k1…
🌊 Tsunami hazina msimu na zinaweza kutokea ghafla.
Ukihisi tetemeko kubwa la ardhi au kuona bahari ikirudi nyuma, usisubiri onyo. Elekea eneo la juu au mbali na pwani.
Katika #TsunamiDay, @UNDRR inatukumbusha kuwa kujiandaa kunaokoa maisha. tsunamiday.undrr.org
Hakuna mtoto anayepaswa kuogopa kwenda shule au kutumia mtandao.
Ukatili na uonevu huathiri afya, ustawi na elimu ya watoto.
Leo, @UNESCO inatukumbusha kuwa wazazi, walimu na jamii lina jukumu la kuhakikisha kila mtoto anajifunza kwa usalama na heshima. unesco.org/en/days/against-s…
Kutoka kwa wavuvi wanaotegemea maji hadi dubu wa Aktiki na radi zinazomulika anga!
Picha hizi zilizoshinda shindano la kalenda ya 2027 la @wmo zinaonyesha uzuri na maajabu ya hali ya hewa, maji na tabianchi duniani.
Angalia zingine hapa: flickr.com/photos/worldmeteo…
Njaa inazidi kutishia maisha nchini Somalia.
Zaidi ya watu milioni 5 wanakabiliwa na uhaba wa chakula, huku karibu watoto milioni 2 wakiwa hatarini kupata utapiamlo mkali.
@WFP inahitaji ufadhili wa haraka kuendeleza msaada wa kuokoa maisha. wfp.org/emergencies/somalia
Hakuna anayepaswa kuhatarisha maisha yake kwa kutafuta usalama.
Kwa watu wanaokimbia vita, vurugu na mateso, kutafuta hifadhi ni haki ya msingi ya binadamu na matumaini ya kuanza maisha upya.
Angalia @UNHCR inafanya nini: unhcr.org/us/what-we-do






















